Promoting Domestic Tourism Through Sports.

Sunday, October 28, 2012

Mbio za Rock City Marathon 2012 zafana

Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 497 walijitokeza kushiriki mashindano hayo. Na Mwandishi wetu Mwanza
Mwanariatha Kopiro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo. Na Mwandishi wetu Mwanza.

Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na mwandishi wetu Mwanza.
Wanariadha kutoka nchi za kigeni wakishiriki  mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na mwandishi wetu Mwanza.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na mwandishi wetu Mwanza.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na mwandishi wetu Mwanza.

Mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon 2012, Mwita Kopiro Marwa kutoka Mwanza aliyejishindia medali ya dhahabu na kitita cha shilingi 1,200,000/=,akiwa na uso wa furaha mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo na mwakilishi wa NSSF. Mbio hizo zilifanyika jana jijini Mwanza
Mshindi kwa mbio za kilomita 2 watoto upande wa wavulana Iddy Suguta kutoka mkoani Mara akiwa na medali yake ya dhahabu pamoja na fedha kwenye bahasha
Mwanamuziki toka Bongo Fleva Baby Madaha akitoa burudani kwa wakazi wa jiji la Mwanza waliohudhuria mashindano ya Rock City marathon kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Jane Matinde ambaye ni Afisa uhusiano wa Airtel amewashukuru wakazi wa Mwanza kwa kujitokeza kwenye michuano ya Rock City Marathon 2012 pamoja na kushukuru waandaji wa mbiyo hizo, kampuni ya Capital Plus International, kwa kuweza kufanikisha mashindano hayo, sambamba na kuweka bayana mpango ya siku za usoni ya Airtel katika kuendeleza na kukuza michezo mbalimbali hapa nchini.
===================================================

MWANARIADHA  Kopiro Mwita kutoka Mwanza na Mary Naaly kutoka Arusha  wameibuka vinara katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili.
Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume baada ya kuchukua saa 1:04:02 huku mwanadada Naaly akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa 1:16:33. Zaidi ya wanariadha 497 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.
Dotto Ikangara kutoka Arusha alingara katika mbio za kilometa tano kwa upande wa wanaume, akinpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili  na Paul Elias Kutota Ukerewe alishika nafasi ya tatu.
Mbio hizi ambazo zimekuwa zikiandaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, kwa mwaka huu ulidhaminiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF), Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, Shirika la Ndege la Air Tanzania, Parastal Pension Fund (PPF), African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), ambao waliwezesha uboreshaji wa tuzo kwa washiriki.
Washiriki na washabiki wa mbio za Rock City za mwaka huu walipata kuburudishwa na msanii maarufu wa Tanzania Juma Nature a.k.a Sir Nature na kundi lake la TMK Wanaume akishirikiana na Baby Madaa katika kuimba wimbo wao mpya “Narudi Nyumbani” ambayo wameimba kwa mara ya kwanza Mwanza.          
Rais wa Shirikisho cha Riatha Tanzania, Anthony Mtaka, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi mbali na kutoa onyo kwa wanaovamia viwanja vya michezo, alionyesha kurithika na jinsi maandalizi na usimamizi wa mbio hizi za Rock City Marathon ya mwaka huu ilivyofanyika, huku akiongeza kuwa  mbiyo hizi imeweza kuibua vipaji vingi vya riadha ambayo vinahitaji kukuzwa.
“Mawashukuru sana waandaaji wa mbiyo hizi za Rock City Marathon kwa kuweza kuandaa shindano ambalo limeweza kutusaidia sisi wadau wa riadha kugundua vipaji vingi ambavyo tunavyo hapa nchini. Hivi vipaji vinastahili kukuzwa. Hivyo basi natoa wito kwa makampuni, mashirika na hata serikali kuweza kudhamini mashindano kama haya mabayo yanasaidia sana kuendeleza na kuibua vipaji vingi vya mchezo wa riatha hapa nchini,” alisema.
Mtaka alisema mbio za Rock City Marathon imeonyesha kiwango kikubwa ambapo aliongeza kuwa inaleta ushindani mkubwa kwa mbio za Kilimanjaro Marathon ambayo imekuwa inakimbizwa kwa miaka mingi .
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa Vyama vya riadha Tanzania (AT) Suleiman Nyambui alisema Rock City Marathon imeonyesha kukuwa kila mwaka, kwa kuwa inauwezo wa kikimbiza mbio za ngazi zote; nusu marathon, kilometa tano, kilometa tatu kwa walemavu, kilometa tatu kwa wazee na kilometa mbili kwa watoto.
Washiriki kutoka mikoa mbali mbali waliweza kushiriki na wageni kutoka nchi kama India, Canada, Australia, Africa Kusini, Rwanda, Kenya and Uganda pia walishiriki.
Mbali na medali walizipata washindi hawa, zawadi ya fedha taslimu zilitolewa ambapo washidi wa pili katika mbio za kilometa 21, upande wa wanaume an wanawake walipata 900,000/- kila mmoja. 
Washindi wa tatu kilometa 21 wakiondoka na 700,000/- kila mmoja na wan ne hadi wa 10 walizawadiwa 150,000/- kila mmoja. Wale wakioshika nafasi ya 11 hadi 25 waliondoka na 100,000/- kila mmoja kwa upane wa wanaume na wanawake.
Jeremiah Kinshuzi kutoka Mwanza aliyeshinda kilometa tatu kwa upande wa wazee na Pascal Emanuel kutoka Kisese kwa upande wa watu wenye ulemavu walizawadiwa 50,000/= kila mmoja, huku washindi wa pili wakiondoka na 30,000/=, na washindi wa tatu wakizawadiwa 20,000/= kilammoja, bila kuwasahau wale alioshika nafasi kati ya nne na 25 ambao walizawadiwa 15,000/= kila mmoja.
Kwa upande wa watoto ambao walikimbia kilometa mbili, Idd Suguta kutoka  Mara na Emma Imhoff kutoka Singida waliibuka washindi na kuzawadiwa  30,000/= kila mmoja, huku washindi wa pili wakipata 20,000/= na watatu 15,000/=,na  walioshika nafasi ya nne hadi 25 wakapata kifuta jasho cha 10,000/= kila mmoja.