Mwanariatha Kopiro Mwita kutoka Mwanza
akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa
upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon
2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi
1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na
kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo. Na
Mwandishi wetu Mwanza.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock
City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/=
ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga
kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na
mwandishi wetu Mwanza.
Wanariadha kutoka nchi za kigeni
wakishiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana
vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital
Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano
hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na mwandishi wetu Mwanza.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock
City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/=
ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga
kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na
mwandishi wetu Mwanza.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock
City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/=
ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga
kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza jana. Picha na
mwandishi wetu Mwanza.
Mshindi
wa kwanza wa mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon 2012, Mwita Kopiro Marwa
kutoka Mwanza aliyejishindia medali ya dhahabu na kitita cha shilingi
1,200,000/=,akiwa na uso wa furaha mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo na
mwakilishi wa NSSF. Mbio hizo zilifanyika jana jijini Mwanza
Mshindi
kwa mbio za kilomita 2 watoto upande wa wavulana Iddy Suguta kutoka mkoani Mara
akiwa na medali yake ya dhahabu pamoja na fedha kwenye bahasha
Mwanamuziki toka Bongo Fleva Baby
Madaha akitoa burudani kwa wakazi wa jiji la Mwanza waliohudhuria mashindano ya
Rock City marathon kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Jane Matinde ambaye ni Afisa
uhusiano wa Airtel amewashukuru wakazi wa Mwanza kwa kujitokeza kwenye michuano
ya Rock City Marathon 2012 pamoja na kushukuru waandaji wa mbiyo hizo, kampuni
ya Capital Plus International, kwa kuweza kufanikisha mashindano hayo, sambamba
na kuweka bayana mpango ya siku za usoni ya Airtel katika kuendeleza na kukuza
michezo mbalimbali hapa nchini.
===================================================
MWANARIADHA Kopiro Mwita
kutoka Mwanza na Mary Naaly kutoka Arusha wameibuka vinara katika
mashindano ya riadha ya kilometa 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon
2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili.
Mwita alishinda mbio hizo kwa upande
wa wanaume baada ya kuchukua saa 1:04:02 huku mwanadada Naaly akishinda kwa
upande wa wanawake baada ya kutumia saa 1:16:33. Zaidi ya wanariadha 497
walijitokeza kushiriki mashindano hayo.
Dotto Ikangara kutoka Arusha
alingara katika mbio za kilometa tano kwa upande wa wanaume, akinpiku John
Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili na Paul Elias Kutota
Ukerewe alishika nafasi ya tatu.
Mbio hizi ambazo zimekuwa
zikiandaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, kwa
mwaka huu ulidhaminiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF), Airtel
Tanzania, Geita Gold Mine, Shirika la Ndege la Air Tanzania, Parastal Pension
Fund (PPF), African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza
Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), ambao waliwezesha uboreshaji wa
tuzo kwa washiriki.
Washiriki na washabiki wa mbio za
Rock City za mwaka huu walipata kuburudishwa na msanii maarufu wa Tanzania Juma
Nature a.k.a Sir Nature na kundi lake la TMK Wanaume akishirikiana na Baby
Madaa katika kuimba wimbo wao mpya “Narudi Nyumbani” ambayo wameimba kwa mara
ya kwanza Mwanza.
Rais wa Shirikisho cha Riatha
Tanzania, Anthony Mtaka, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi mbali na kutoa onyo kwa
wanaovamia viwanja vya michezo, alionyesha kurithika na jinsi maandalizi na
usimamizi wa mbio hizi za Rock City Marathon ya mwaka huu ilivyofanyika, huku
akiongeza kuwa mbiyo hizi imeweza kuibua vipaji vingi vya riadha ambayo
vinahitaji kukuzwa.
“Mawashukuru sana waandaaji wa mbiyo
hizi za Rock City Marathon kwa kuweza kuandaa shindano ambalo limeweza
kutusaidia sisi wadau wa riadha kugundua vipaji vingi ambavyo tunavyo hapa
nchini. Hivi vipaji vinastahili kukuzwa. Hivyo basi natoa wito kwa makampuni,
mashirika na hata serikali kuweza kudhamini mashindano kama haya mabayo
yanasaidia sana kuendeleza na kuibua vipaji vingi vya mchezo wa riatha hapa
nchini,” alisema.
Mtaka alisema mbio za Rock City
Marathon imeonyesha kiwango kikubwa ambapo aliongeza kuwa inaleta ushindani
mkubwa kwa mbio za Kilimanjaro Marathon ambayo imekuwa inakimbizwa kwa miaka
mingi .
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa
Vyama vya riadha Tanzania (AT) Suleiman Nyambui alisema Rock City Marathon
imeonyesha kukuwa kila mwaka, kwa kuwa inauwezo wa kikimbiza mbio za ngazi
zote; nusu marathon, kilometa tano, kilometa tatu kwa walemavu, kilometa tatu
kwa wazee na kilometa mbili kwa watoto.
Washiriki kutoka mikoa mbali mbali
waliweza kushiriki na wageni kutoka nchi kama India, Canada, Australia, Africa
Kusini, Rwanda, Kenya and Uganda pia walishiriki.
Mbali na medali walizipata washindi
hawa, zawadi ya fedha taslimu zilitolewa ambapo washidi wa pili katika mbio za
kilometa 21, upande wa wanaume an wanawake walipata 900,000/- kila mmoja.
Washindi wa tatu kilometa 21
wakiondoka na 700,000/- kila mmoja na wan ne hadi wa 10 walizawadiwa 150,000/-
kila mmoja. Wale wakioshika nafasi ya 11 hadi 25 waliondoka na 100,000/- kila
mmoja kwa upane wa wanaume na wanawake.
Jeremiah Kinshuzi kutoka Mwanza
aliyeshinda kilometa tatu kwa upande wa wazee na Pascal Emanuel kutoka Kisese
kwa upande wa watu wenye ulemavu walizawadiwa 50,000/= kila mmoja, huku
washindi wa pili wakiondoka na 30,000/=, na washindi wa tatu wakizawadiwa
20,000/= kilammoja, bila kuwasahau wale alioshika nafasi kati ya nne na 25
ambao walizawadiwa 15,000/= kila mmoja.
Kwa upande wa watoto ambao
walikimbia kilometa mbili, Idd Suguta kutoka Mara na Emma Imhoff kutoka
Singida waliibuka washindi na kuzawadiwa 30,000/= kila mmoja, huku
washindi wa pili wakipata 20,000/= na watatu 15,000/=,na walioshika
nafasi ya nne hadi 25 wakapata kifuta jasho cha 10,000/= kila mmoja.
|
No comments:
Post a Comment